Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba Jiji FC wazindua Jezi mpya

Pamba Jiji Jezi Pamba Jiji FC wazindua Jezi mpya

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Pamba Jiji Fc ya Jijini Mwanza inayoshiriki michuano ya NBC Championship imezindua jezi za msimu wa 2023/2024 uzinduzi ambao umekwenda sambamba na ufunguzi wa duka la Pamba na duka linalotembea (mobile shop) jezi moja itauzwa Tsh 30,000 kila mauzo ya jezi moja Klabu inapata Tsh 8000.

Jezi hizo zimetengenezwa na Kampuni ya Netsport zimezinduliwa Oktoba 6,2023 saa 3 usiku katika jengo la Rock City Mall, Jijini Mwanza.

Jezi za nyumbani ni rangi ya kijani, jezi ya ugenini ni rangi nyeupe jezi ya tatu rangi ya blue.

Akizindua jezi hizo mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Sima Constantine amesema uzinduzi wa jezi hizo utachangia kuinua uchumi wa timu yao huku akiwataka mashabiki wa klabu hiyo kote nchini kununua kwa wingi jezi hizo ili kuchangia mapato ya klabu.

Kwa upande wake mmoja wa Wakurugenzi wa Netsport, Darius Bujaga amesema hatua hiyo ni safari ya kufanya mapinduzi ya mpira wa miguu kwa klabu hiyo yenye heshima nchini na inastahili kuwa mahali fulani kwa sasa.

Nae Mtendaji Mkuu wa klabu ya Pamba Jiji, Wakili msomi Alhaj Majogoro amesema kila mauzo ya jezi moja klabu inapata mgao wa Tsh 8000 ambae amewaomba wadau na mashabiki kununua jezi kwa wingi kuichangia timu hiyo na akasema kiasi hicho ni kikubwa kuwahi kutolewa kwa timu kwenye mauzo ya jezi Tanzania.

Katika uzinduzi huo pia walikuwepo Viongozi mbalimbali wa Serikali ya mkoa, viongozi wa michezo na wachezaji wa zamani wa klabu ya Pamba, na wadau wa michezo mkoa wa Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: