Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pale juu vita imeanza kunoga

Pale Juu Pale juu vita imeanza kunoga

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Msimamo wa La Liga unavyosoma, Real Madrid imezidi kujiimarisha kileleni baada ya kujikusanyia pointi 65 katika mechi 26.

Barcelona imeonyesha kuwa ukubwa dawa baada ya kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo huo kwa kuwa na pointi 57 katika mechi 26, lakini hiyo ni kabla ya mchezo wa Girona na Rayo Vallecano iliyotarajiwa kufanyika usiku wa jana Jumatatu.

Girona ilikuwa na pointi 56 katika mechi 25. Ushindi wa nyumbani dhidi ya Rayo, utawarudisha kwenye nafasi ya pili katika msimamo huo wa La Liga na kuendeleza mapambano kuwania taji na Los Blancos.

Wakati mchakamchaka huo wa La Liga ukiingia kwenye mechi ya 26, kilichovutia wengi wikiendi iliyopita ni kitendo cha Barcelona kupata matokeo ya kibabe dhidi ya Getafe na kupunguza pengo la pointi dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Real Madrid. Na sasa pengo ni pointi nane.

Ijumaa kulikuwa na mechi moja, ambapo Villarreal iliiduwaza Real Sociedad kwa kipigo cha mabao 3-1 na kufikisha pointi 29 zinazowafanya kuwa mbali na shimo la kushuka daraja, huku wakipata ushindi wa saba msimu huu.

Barca mipango mingi

Barcelona chini ya kocha wake Xavi Hernandez, ambaye ataachia ngazi mwishoni mwa msimu, ilionyesha kandanda matata kabisa na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Getafe.

Raphinha, Joao Felix, Frenkie De Jong na Fermin Lopez walikuwa masteringi wa mchezo katika mechi hiyo, wote wakitikisa nyavu na kuipa ushindi muhimu ambao Barcelona iliuhitaji.

Ushindi huo si tu kwamba umerudisha morali kwa Barca, bali kuimarisha nafasi kwenye msimamo na kurejea kwenye vita ya kuwania ubingwa. Pointi 57, zinawafanya kuwa nyuma kwa pointi nane dhidi ya vinara, Real Madrid baada ya ushindi mbele ya Sevilla, shukrani kwa bao pekee la Luka Modric.

Vita ya ubingwa

Wakati ligi ikiendelea, vita ya kusaka ubabe kwenye La Liga inazidi kupamba moto. Real Madrid, licha ya kuongoza ligi, haipaswi kuteleza, kwasababu Barcelona wapo nyuma yao wanakuja kwa kasi.

Girona, wababe wengine walioshangaza msimu huu, nao bado wapo kwenye mbio za ubingwa na kama watakuwa wameshinda mchezo wa usiku wa jana Jumatatu dhidi ya Rayo Vallecano watakuwa wamepunguza pointi la pointi kwa kiasi kikubwa na kuwakaribisha Los Blanhcos kileleni.

Kwingineko, Alaves na Mallorca zilitoka sare ya 1-1, huku Almeria pia ikiigomea Atletico Madrid na kufungana mabao 2-2 katika mchezo uliofanyika Estadio Mediterraneo. Real Madrid iliibuka na ushindi muhimu kabisa wa bao 1-0 dhidi ya Sevilla, unawafanya waendelee kujitanua kwenye kilele cha ligi hiyo.

Real Betis inakuja

Betis imepiga hatua muhimu katika msako wao wa kucheza soka la Ulaya msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao, ambayo ilikuwa na wachezaji 10 uwanjani.

Bao la Ezequiel Avila na lile la kujifunga la Yuri Berchiche yalitosha kuipa Betis kukaa matamu kabla ya mkali wa Athletic, Nico Williams kuonyeshwa kadi nyekundu na hapo ikatoa unafuu zaidi kwa Betis.

Na licha ya kwamba Athletic ilijaribu kufunga bao moja, Johnny Cardoso alimaliza mechi kwa kufunga bao la tatu na kuifanya kupanda kwenye nafasi ya sita katika msimamo wa La Liga, wakiendelea na vita yao ya kusaka tiketi ya michuano ya Ulaya msimu ujao. Matokeo mengine, Cadiz na Celta Viga zilitoka sare ya 2-2 na Las Palmas na Osasuna nazo zilifungana 1-1.

Chanzo: Mwanaspoti