Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome na Ngoma ni mbingu na ardhi - Shabiki Simba

Ngoma Pacome Pacome na Ngoma.

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa aliyemshauri mchezaji wa timu hiyo, Fabrice Ngoma kupaka bleach ili afanane na Pacome Zouzoua wa Yanga alikosea sana.

Ngoma ambaye ni raia wa Congo DR anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji ndani ya Wanalunyasi alionekana kuwa amebadilisha muonekano wake na kupaka bleach nywele zake wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

"Ndio maana hata Yanga akitusema ni sawa, Ngoma kapaka bleach kama ya Pacome na kaenda kuchezeshwa namba 10 ya Pacome, ina maana ni kweli walitaka kumfananisha Ngoma na Pacome. Ni sahihi kiungo mchezeshaji kumfananisha na kiungo namba 10?

"Sijajua malengo ya kumfananisha Ngoma na Pacome yalikuwa ni yapi lakini ukiangalia uhalisia, utagundua Ngoma na Pacome walitaka kufanana kimuonekano lakini uwanjani ni mbingu na ardhi, Ngoma yupo slow sana," amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: