Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome kuwavaa TS Galaxy

Gamondi Chama Aziz Pacome Pacome kuwavaa TS Galaxy

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua amejiunga na kambi ya kikosi cha Klabu yake nchini Afrika Kusini akitokea kwao Ivory Coast alikokuwa amekwenda kufuatilia hati yake ya kusafiria.

Klabu ya Yanga inatarajia kushuka Dimbani siku ya kesho Jumaa tano 24/2024 majira ya saa 10:00 kumenyana na TS Galaxy kwenye mchezo wa kirafiki.

Viungo Khalid Aucho na Pacome Zouazoa ambao waliokosekana katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ausburg watashiriki mchezo huo.

"Na taarifa njema ni kwamba mchezaji wetu Pacome Zouzoua amerudi kwenye kiwanja cha mazoezi na tunatarajia kuwa nae katika mchezo huo," amesema Ally Kamwe.

Kocha wa yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa katika mchezo huo ujao atawapa nafasi wachezaji wake wote angalau dakika 45 kila mmoja ili kutengeneza fitness.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: