Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome hana kipaji kama Chama - mchambuzi

Pacome Chama Pc Pacome hana kipaji kama Chama - mchambuzi

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Alex Ngereza amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua hana kipaji kikubwa kama kiungo wa Simba, Clatous Chama.

Ngereza amesema kuwa, kinachombeba Pacome ni kujituma kwake na si kipaji kama watu wanavyodhani kuwa anamzidi Chama.

Pacome juzi alionyesha kiwango bora kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afika dhidi ya CR Baleouizdad uliopewa jina la Pacome Day na kifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 4-0 na kutinga hatua ya robo fainali huku mwamba huyo kutoka Ivry Coast akiwatesa Waarabu na kutoa assist.

"Pacome Zouzouan hana kipaji kikubwa cha mpira kama Chama ila anajituma kuliko Chama. Ndio kwenye statistic msimu amefunga magoli matatu na assist moja kwenye michuano ya Klabu Bingwa Barani Africa tena kwenye group stage.

"Hawa wachezaji wote wawili wanaweza kucheza kwenye eneo moja lakini wanatofautiana kuna mmoja ana kipaji kikubwa cha mpira na mwingine ana kidogo ila anajituma zaidi kuliko mwenzake hawana tofauti na Messi na Ronaldo," amesema Alex.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: