Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome hajaenda Sauzi na Yanga, yuko wapi?

Aziz Chama Pacome Yanga 3 Pacome hajaenda Sauzi na Yanga, yuko wapi?

Sat, 20 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya sintofahamu ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua kutoongozana na kikosi cha timu hiyo kwenda Afrika Kusini, Nimefichuliwa sababu iliyomfanya asiwe sehemu ya kikosi hicho ni ishu ya pasipoti, na amepewa siku tano kumaliza tatizo hilo kabla ya kuungana na wenzake Sauzi.

Awali kiungo huyo alikuwa pamoja na kikosi hicho tangu mazoezi hayo ya Pre Season kuanza, lakini juzi wakati timu uinaoondoka hakuwepo na ilishindikana kufahamika kwa mapema, hadi jana ilipoelezwa tatizo lililoomzuia asiondoke na wenzake ni pasipoti na amepewa siku tano kuanzia leo kuishughulikia.

“Sababu ya Pacome kutoondoka pamoja na wenzake ni pasipoti yake ilikuwa imejaa, hivyo inatakiwa arejee nchini kwao Ivory Coast kwaajili ya kupata nyingine,” kilisema chanzo changu kutoka Yanga na kuongeza:

“Kutokana na umuhimu wa sababu yake, uongozi umempa siku tano, ili akamilishe kila kitu, kisha ajiunge na wenzake Afrika Kusini, ambako watakaa wiki mbili na kurejea nchini kujiandaa na mambo mengine.” Hivyo kwenye mchezo wa leo wa Kirafiki dhidi ya Ausburg ya Ujerumani Mwamba hatokuwepo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live