Kuelekea mchezo wa kirafiki kati ya Ivory Coast dhidi ya Benin Machi 23 na Uruguay Machi 26 kiungo wa miamba hiyo ya Africa Pacome Zouazoua amewekwa kwenye kundi la nyota wanaofanya mazoezi mepesi.
Ikumbukwe nyota huyu alipata jeraha la Goti kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC na baadae alipopata wito wa timu ya Taifa licha ya majeraha yake Ivory Coast walitaka kwenda kumuangalia kwa ukalibu zaidi.
Nyota huyu mpaka sasa bado haijawa rasmi kama ataweza kucheza michezo hiyo ya Ivory Coast na ule wa mkondo wa kwanza wa klabu yake kwenye Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.