Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome ataja sababu za kuomba kucheza dabi

Yanga Tano Pacome Maxi 191929 Pacome ataja sababu za kuomba kucheza dabi

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua afunguka sababu zilizomfanya amuombe kocha wake Miguel Gamondi ili acheze mechi ya Dabi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya watani zao, Simba, juzi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pacome amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo ndani ya kikosi cha Yanga, lakini amekuwa nje tangu alipoumia katika mechi dhidi ya Azam alipotolewa dakika 28 ya kipindi cha kwanza.

Katika mechi ya kwanza ya ligi Yanga ilipokutana na Simba na kushinda mabao 5-1, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofunga akiwa ametia nyavuni bao la mwisho kwa timu yake dakika ya 86.

Akizungumza na Mwanaspoti, ameeleza kuwa licha ya majeraha aliyonayo alitaka kusaidia timu yake bila kujali anapitia changamoto gani.

Mmoja wa mabosi wa Yanga aliieleza Mwanaspoti juzi kuwa baada ya Pacome kuwasilisha ombi hilo kwa Gamondi, kocha huyo hakukubali.

Kikosi hicho kilipowasili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kiungo huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji walioukagua uwanja huo na alionekana muda wote kuwa mchangamfu huku akicheza.

Hata hivyo, akizungumza na Mwanaspoti Pacome ameeleza kuwa sababu kuwa ni kwamba alikuwa anaumia kuona mashabiki wa Yanga wanatamani kumuona anarejea uwanjani ili aisaidie timu hiyo kwenye mchezo huo mgumu, hivyo alimuoma kocha wake ampatie dakika kadhaa ili acheze.

Amesema amekosa mechi nyingi muhimu jambo ambalo linamkosesha amani na kumfanya apoteze rekodi yake nzuri aliyoweka kutokana na michezo ya aina hiyo.

"Najua mashabiki wanatamani kuniona uwanjani lakini mimi mwenyewe natamani kurejea kuitetea timu yangu, ile ni mechi kubwa na yenye presha kubwa hivyo kwangu haikuwa rahisi kuona naendelea kukaa nje," amesema Pacome ambaye ni kiungo wa zamani wa ASEC Mimosas.

"Kocha alikataa na kuniambia nijipe muda zaidi nipone sawasawa kwani wapo wenzangu watafanya vizuri, nilikubali na kumuelewa kocha ingawa roho ilikuwa inaniuma ila kikubwa tumepata ushindi."

Yanga ipo kileleni katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 58 ilizokusanya katika mechi 22, huku ikishinda mechi 19, sare moja na kufungwa mbili.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: