Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome anawakata kiu Wananchi

Pacome X Al Ahly Pacome anawakata kiu Wananchi

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miaka kadhaa iliyopitaa Simba SC walikuwa wanatamba na uwepo wa utajiri katika idara ya kiungo mshambuliaji wakati huo idara ya viungo washambuliaji ikiwa na Chama, Bwalya, Dilunga, Miquissone na tukawaona Simba wakiwa tishio sio ndani tuu hata nje.

Hawa viungo na wengineo waliifanya Simba SC wacheze soka la kuvutia kweli kutokana na bora waliokuwa nao waliokuwa nao na combination ya ya hatari ukijumlisha na wakina Jonas Mkude, Fraga baadae Thadeo Lwanga Simba ilikuwa ya moto kweliii.

Jambo lililowafanya mashabiki na viongozi wa Yanga SC kutamani kuwa na kiungo kama Chama mara kadhaa ilielezwa kuiwinda saini yake lakini hadi leo hawajafanikiwa bado Chama ni Lunyasi.

Nafikiri hata ujio wa Aziz Ki wanayanga wengu waliamini kuwa atakuja kupika kile anachopika Mwamba wa Lusaka pale Msimbazi bahati mbaya msimu wake wa kwanza haukuwa mzuri.

Msimu huu Yanga SC walifanikiwa kumsajili kiungo fundi wa boli kutokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Pacome ZouZoua usajili wake haukuwa na mbwembwe nyingi kama ilivyokuwa kwa Aziz Ki lakini huyu ndie aliyekata kiu ya Wananchi kuwa na kiungo Sampuli ya Chama.

Kwanza Pacome ana ufundi wa hali ya juu sana ni mbunifu anajituma dakika zote 90 kama amekunywa maji ya bendera ya wananchi, anafanya Football ionekane mchezo mrahisi sana cha ziada ambacho amebarikiwa na nitofauti na viungo wengi washambuliaji ni uwezo wake wa kukaba hii ni silaha kubwa kwake na Yanga SC kwa ujumla.

Nafikiri Pacome anawakata wananchi kiu yao ya kuwa na kiungo fundi kama Clotaus Chama 'Mwamba wa Lusaka'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live