Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome aitwa Timu ya Taifa

Pacome 1 Goal Pacome aitwa Timu ya Taifa

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga Sc, Pacome Zouzoua, ameitwa kwenye timu ya Taifa ya Ivory Coast ambao ni mabingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2023) kuchukua nafasi ya Ibrahim Sangare wa Nottingham Forest ya Uingereza aliyepata majeraha.

Pacome ameitwa huku akiwa amepata majereha katika mchezo wa Dar es Salaam Derby baina ya Azam FC dhidi ya timu yake ya Yanga na kulazimika kutolewa nje.

Kiungo mshambuliaji mwingine wa Ivory Coast, Seko Fofana naye ana amajeraha, hivyo Kocha Emerse Fae anapambana kupata mbadala atakayemsaidia kutimiza majuku kwenye kikosi chake.

Ikumbukwe kuwa Pacome Zouzoua, hakumaliza mchezo wa DarDerby baina ya Azam FC dhidi ya Yanga SC baada ya mchezaji huyo kupata majeraha na kulazimika kutolewa nje kwa lazima.

Je! Yanga wataruhusu Pacome akajiunge na mabingwa wa Afrika 2023/2024?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live