Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome afunguka kuhusu Mamelodi

Pacome Ivorys Pacome afunguka kuhusu Mamelodi

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati mashabiki wengi wakijiuliza kuhusu hatma ya staa wa Yanga, Pacome Zouzoua kama atakuwepo katika mechi dhidi Mamelodi kutokana na majeraha aliyoyapa hivi karibuni, mwenyewe amewatoa wasiwasi akisema: "Msijali Wananchi nipo fiti."

Pacome aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC na kutolewa katika dakika ya 28 kipindi cha kwanza na kuzua hofu kwa mashabiki na viongozi wa Yanga ambao macho na akili zao zipo kwenye mechi muhimu ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pacome ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi hicho, licha ya kuanza kukitumikia msimu huu akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast, amekuwa na rekodi nzuri tangu atue klabuni hapo.

Katika hatua ya makundi Yanga ilicheza mechi sita, huku kiungo huyo akihusika na mabao manne akifunga matatu na kutoa asisti moja kati ya tisa ya timu yake na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika michuano hiyo ndani kikosi hicho. Pacome pia anashika nafasi ya pili katika orodha ya vinara wa mabao wa Ligi ya Mabingwa msimu huu akizidiwa bao moja tu na Sankara Karamoko aliyekuwa Asec Mimosas kabla ya kutimkia Ulaya ambaye alifunga mabao manne.

Akizungumza na Mwanaspoti akiwa nchini Ufaransa alikokwenda kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa, alisema anaona jinsi mashabiki wanavyotamani kumuona tena uwanjani hasa katika mechi hiyo muhimu.

"Kwa sasa najisikia vizuri, naweza kusema nipo fiti, kama hali yangu itaendelea hivi basi nitacheza mechi dhidi ya Mamelodi, na ninatamani kuendelea kutunza rekodi yetu ya kushinda uwanja wa nyumbani japo wapinzani wetu nao wana kikosi bora.

"Tunakutana timu zote ambazo ni bora, ndiyo maana tunashiriki michuano mikubwa kama hii na mipango yetu ni kama ikiwa hivyo basi tutakuwa na morali kubwa ya kutinga nusu fainali kwani takuwa tumeshajihakikishia nafasi hiyo.

Aliongeza kuwa:"Nawaomba mashabiki wafike kwa wingi uwanjani ili kushabikia timu yao kwani uwepo wao unaongeza nguvu kubwa hasa kwetu sisi wachezaji," alisema Pacome.

Ukiachana na Pacome kiungo, Khalid Aucho naye anaendelea vizuri na tayari ameshajiunga na kikosi hicho jana akiendelea na mazoezi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: