Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome aanza tizi kali Timu ya Taifa

Pacome Ivorys Pacome aanza tizi kali Timu ya Taifa

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua ameanza mazoezi ya pamoja ya Timu ya taifa ya Ivory Coast.

Hiyo ikiwa saa chache tangu ajiunge na kikosi cha timu hiyo, ambacho kimeweka kambi nchini Ufaransa kikijiandaa na michezo ya kirafiki dhidi ya Benin na Uruguay.

Pacome ambaye aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC weekend iliyopita dhidi ya Azam Fc na kulazimika kutolewa nje mapema kipindi cha kwanza, jana amefanya mazoezi kwa ufanisi mkubwa na timu yake ya Taifa.

Hii inaondoa mashaka kwa Kocha Miguel Gamondi na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa na hofu iwapo atakuwa sehemu ya kikosi cha Wananchi mnamo Machi 30, watakapovaana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika Dimba la Mkapa kwenye mchezo wa robo fainali ya CAFCL.

Wachezaji wengine wa Yanga ambao bado wapo kwenye majeraha ni Khalid Aucho ambaye amefanyiwa upasuaji mdogo wa goti, Kouassi Yao, Kibwana Shomari na Zawadi Mauya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live