Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome, Yao waliamsha Yanga, Gamondi atoa msimamo

Yao Pacomereg HD Pacome, Yao waliamsha Yanga, Gamondi atoa msimamo

Sun, 14 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastaa wa Yanga ambao hawapo katika timu zao za taifa zinazoshiriki fainali za Afcon 2023, akiwamo Pacome Zouzoua na Yao Kouassi wameliamsha kwenye mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara, Kombe la ASFC na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pacome na wenzake walianza mazoezi ya gym tangu juzi na kesho wataanza rasmi kujifua uwanjani baada ya kocha mkuu wa timu hiyo kuwaagiza kuripoti kambini haraka ili kuendelea na mipango mipya ikiwa ni siku chache tangu itolewe kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024.

Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko kupisha michuano ya Mapinduzi iliyofikia tamati jana kwa kupigwa fainali baina ya Simba na Mlandege na kocha aliwapa ratiba ya kuanzia gym wakiwamo wale waliokuwa wagonjwa na majeruhi kabla ya wote kesho kuanza mazoezi ya uwanjani.

Yanga inarudi kambini ikiwa na kibarua kizito cha mechi mbili za makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria na Al Ahly ya Misri, huku ikiwa na kiporo cha ASFC na Hausing ya Njombe mbali na Ligi Kuu ambapo timu hiyo ipo nafasi ya pili kwa sasa katika msimamo.

Licha ya mazoezi hayo kuanza rasmi kesho, Yanga haitakuwa na nyota 11 wengi wao wa kikosi cha kwanza kutokana na kushiriki fainali za Afcon 2023 wakiwa na timu tofauti.

Wachezaji watakaokosekana watakaosubiriwa hadi fainali hizo za Ivory Coast ziishe ili waungane na wenzao kambini ni kipa namba moja Djigui Diarra (Mali), mabeki Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca na kiungo Mudathir Yahya (wote Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso), Mzambia Kennedy Musonda.

Akizungumza nasi, Kocha Gamondi aliweka wazi ratiba timu imeanza mazoezi kujiandaa na michuano iliyopo mbele yao.

“Tunaanza maandalizi  kwenda kuangalia wachezaji wapo kwenye hali gani na tuanze kuimarisha ufiti wao baada ya mapumziko ambayo tumewapa,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Wapo wachezaji walioanza mazoezi mepesi na kocha wa viungo ambao ni wale waliokuwa majeruhi na wanaendelea kwa sasa vizuri kwa ripoti nilizopewa, tunaanza maandalizi mapema ili tupate muda wa kurudisha ubora, ligi ikirejea itakuwa na ugumu zaidi ni vyema tukawa tayari kwa ushindani.”

ATOA MSIMAMO

Kocha huyo pia ametoa msimamo wa kuutaka uongozi kufanya kila linalowezekana kushusha straika mmoja wa kufungia dirisha dogo.

Yanga inaendelea na msako wa kupata mshambuliaji  a kufungia hesabu zao kabla dirisha dogo halijafungwa rasmi kesho Jumatatu.

Dirisha dogo la usajili linafungwa kesho saa 5:59 usiku ambapo kila timu inahaha kukamilisha maeneo  hayo muhimu ya ufungaji kulingana na upungufu iliyonayo, huku Kocha Gamondi akitaka kuletewa mashine moja ya hatari ili kazi iwe rahisi kwenye michuano wanayoshiriki.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amekaririwa alithibitisha kikosi hicho kitafunga usajili kwa kumuingiza mtu mmoja ingawa hakutaka kutaja nafasi anayocheza mchezaji huyo.

Hata hivyo, Mwanaspoti linafahamu anayekuja ni mshambuliaji.

“Usajili bado na tutamleta mchezaji mmoja kabla ya dirisha la usajili kufungwa,” alisema Hersi wakati akihojiwa na vyombo vya habari baada ya hafla ya harambee ya timu za taifa katikati ya wiki hii.

Hersi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu za Afrika kwa sasa yupo Ivory Coast  ambako amekwenda kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), lakini ikielezwa akiwa na kazi ya kutekeleza agizo la Gamondi la kumshushia straika wa kufunga hesabu baada ya awali kumuingiza Augsutine Okrah kutoka Ghana ambaye aliumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024.

Yanga ndio watetezi wa Ligi Kuu na ASFC ikishikilia mataji hao kwa misimu miwili mfululizo, huku ikiwa inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D la Ligi ya Mabingwa ikisaka rekodi nyingine ya kwenda robo fainali, kwani haijawahi kufanya hivyo tangu michuano hiyo ilipobadilishwa mwaka 1998.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live