Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome: Wabongo wana balaa kuliko Ivory Coast

Pacome 1 Goal Pacome: Wabongo wana balaa kuliko Ivory Coast

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji Young Africans, Pacome Zouzoua, amesema kuwa mashabiki wa Tanzania wana vibe kubwa na wanazipenda timu zao kuliko ilivyo kwa mashabiki wa nyumbani kwao nchini Ivory Coast.

Pacome amerejea jana dimbani baada ya kukaa nje kwa takribani mwezi na nusu akiuguza majeraha aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC, Machi 17, 2024.

“Tanzania mashabiki wanakuja uwanjani kusapoti timu zao, kitu ambacho nakipenda sana, lakini nyumbani Ivory Coast si rahisi kwa mashabiki kuja uwanjani kutazama mechi, uwapo wa mashabiki unaipa thamani ligi ya Tanzania.”

“Pia mashabiki wanaongeza kitu kwa mchezaji, nimeenda uwanjani kutazama mechi mara mbili kipindi nikiwa majeruhi, watu wananiita na kuniombea nipone haraka na kunipa motisha.

“Hii inanipa nguvu na kuona nina maana kubwa sana kwa hawa watu na kutakiwa kufanya kitu kitakachowapa furaha nitakaporejea uwanjani," amesema Pacome Zouzoua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: