Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome, Mudathir, Kibabage wachuana vikali

Pacome Mudathir Kibabage Pacome, Mudathir, Kibabage wachuana vikali

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwezi Februari ulikuwa wa kihistoria kwa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, baada ya kuvunja ile rekodi iliyodumu kwa miaka 54 kwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Haikuwa tu historia kwa Yanga SC, vilevile nyota kadhaa wa Yanga wakishirikiana na wenzao walionesha viwango maradufu katika kipindi cha mwezi wa pili lengo ikiwa ni kuhakikisha Yanga SC inatimiza malengo yake.

MUDATHIR YAHYA Unapotaja miongoni ya nguzo imara kwenye kikosi cha Miguel Gamondi kwa sasa huwezi kuacha jina la Mudathir Yahya ambaye amekuwa akitumika kama kiungo mchezeshaji.

Takwimu zake mwezi Februari -Goli dhidi ya Kagera Sugar dakika ya 85 -Goli dhidi ya Mashujaa dakika ya 85 -Magoli mawili dhidi ya KMC (1’, 54) -Goli dhidi ya CR Belouzidad dakika ya 43

Katika michezo 5 ya mwezi Februari, Mudathir kwenye dakika 398, amefunga magoli matano.

NICKSON KIBABAGE Mwezi wa pili utabaki kwenye kumbukumbu za Nickson Kibabage akiwa amehusika katika magoli matatu akicheza mechi nne. Licha ya kupata dakika chache ukilinganisha na wenzake, alifanikiwa kutoa pasi tatu muhimu za magoli katika dakika 274 za Ligi Kuu alizocheza.

Alitoa pasi mbili za magoli dhidi ya KMC pale Sokoine, zikaenda kwa Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua kabla ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 71.

Akatoa pasi nyingine kwa Mudathir Yahya kwenye ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, ambapo alitokea benchi dakika ya 72.

Msimu huu Kibabage amefikisha pasi 4 za magoli akiwa mchezaji wa pili kwenye kikosi chetu mwenye asisti nyingi nyuma ya Yao Attohoula mwenye asisti 7. Vilevile katika majukumu yake ya ulinzi, klabu ilifanikiwa kuondoka na cleansheet tatu katika mechi 4 alizocheza.

PACOME ZOUZOUA Ukiachana na burudani ya aina yake aliyotoa dhidi ya CR Belouizidad mwezi Februari, amekuwa na takwimu nzuri ambazo zimeifanya Yanga SC kusalia kileleni mwa Ligi Kuu. Pacome amefunga magoli mawili na kutoa pasi mbili za magoli katika dakika 415.

-Alifunga goli na kutoa pasi ya goli dhidi ya Prisons kwenye ushindi wa magoli 2-1 ikiwa ni moja ya mechi ngumu kule Mbeya.

-Akafunga dhidi ya KMC katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kwenye ushindi wa magoli 3-0.

Kisha akaisambaratisha ngome ya Belouizidad kabla ya kutoa pasi ya goli kwa Kennedy Musonda kwenye ushindi wa magoli manne bila majibu.

Magoli yake mawili muhimu kwenye viwanja vigumu viwili vya ugenini Sokoine na Jamhuri, vinamfanya Pacome kufikisha magoli 6 msimu huu akiwa nafasi ya tatu klabuni.

Ki Aziz Stephane – 10 Maxi Nzengeli – 8 Pacome Zouzoua – 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live