Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome, Maxi wamvuruga kocha Medeama

Pacome X Nzengeli .png Pacome, Maxi wamvuruga kocha Medeama

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga tayari ipo mjini Kumasi, Ghana ikiendelea kujifua kwa ajili ya mechi ya Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika itakapoikabili Medeama kwenye Uwanja wa Baba Yara, huku kocha wa timu wenyeji akitoa kauli juu ya nyota watatu wa mabingwa hao wa Watanzania wakisema wanamuumiza kichwa kwa sasa.

Yanga inavaana na Medeama kesho kuanzia saa 1:00 usiku, ikitoka kulazimishwa sare nyumbani na Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa pili wa kundi hilo baada ya awali kufungwa 3-0 ugenini na CR Belouizdad, huku iki-watesa wenyeji kutokana na aina ya wachezaji walionao kwa sasa kikosini.

Kocha Mkuu wa Medeama, Evance Adotey ameliambia Mwanaspoti wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na tahadhari kubwa kutokana na ubora wa timu wanayokwenda kukutana nao.

Adotey alisema Yanga licha ya kutoshinda mechi yoyote kati ya mbili za kwanza zilizopita bado sio timu wanayotakiwa kuidharau kutokana na ubora wa kikosi chao akiwataja mastaa watatu hatari.

Kocha huyo alisema kwa Yanga ilivyo, kama vijana wake wanataka ushindi wa pili nyumbani wanatakiwa kujipanga kukabiliana na ubora wa viungo wa timu hiyo, waliounda kombinesheni iliyopewa jina la MAP, yaani Maxi Nzengeli, Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua.

“Huwezi kuidharau timu ambayo imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita kwa kigezo cha kutoshinda mechi mbili zilizopita, inawezekana ikawa mechi ngumu nyumbani kuliko ile iliyopita dhidi ya CR Belouizdad,” alisema Adotey na kuongeza;

“Yanga hata kama imetoa sare na kupoteza bado unaona inacheza kama timu bora, wana viungo hatari sana ambao wakati wowote wanaweza kuleta shida eneo lako kama hutajipanga sawasawa. Kuna yule anayevaa jezi namba 10 (Aziz KI), mwingine ni yule jezi namba 7 (Maxi) na hata yule jezi namba 26 (Pacome) ni wachezaji wenye akili kubwa uwanjani, lazima ujue jinsi ya kukabiliana nao kwa nidhamu kubwa.”

“Tunataka kushinda na inawezekana lakini nimewaambia wachezaji wangu kwamba tunatakiwa kujipanga sawasawa kwa kucheza kwa nidhamu kubwa,” al;isisitiza kocha huyo ambaye timu yake inakutana na Yanga kwa mara ya tatu, baada ya awali kuvaana kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho 2016.

Katika mechi mbili za awali dhidi ya Medeama ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na kwenda kulala 3-1, hivyo mchezo wa kesho utakuwa ni wa kulipa kisasi, wakati Waghana wakitaka kuendelea ubabe wakiwa nyumbani kab-kla ya kurudiana wiki ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: