Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome, Maxi waachiwa msala Yanga

Maxi Pacome A0022 Pacome, Maxi waachiwa msala Yanga

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huko Yanga kwa sasa huwaambii kitu na wala hawana maswali tena juu ya suala la ufungaji mabao ndani ya timu hiyo kutokana na viungo wao matata ambao kwa sasa wanatupia mabao ya maana.   Ndani ya Yanga kwa sasa vinara wa upachikaji mabao unashikiliwa na viungo watatu ambao ni Pacome Zouzoua,Maxi Nzegeli na Aziz KI ambao wote kwa pamoja wamefunga mabao matatu katika michezo mitano ambayo Yanga imecheza mpaka sasa.   Sasa kitendo hiko cha viungo hao wa Yanga kufunga mabao yakutosha kimemkuna kocha mkuu Miguel Gamond ambaye anaamini viungo hao watampa mabao ya kutosha na kuwakabidhi jukumu la kuhakikisha wanafunga mabao mengi Zaidi.   “Tunafurahi kuona tuna timu yenye wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao,ukiwa kama kocha lazima ikuvutie kwa kuwa unakuwa na uhakika kuwa utapata mabao mengi.   “Kwa upande mwingine inakuwa nzuri kwa kuwa kuna siku mbaya kazini kutoka kwa washambuliaji basi wao wanakuwa ni msaada mwingine tosha,naamini kwetu Yanga tumejaliwa wachezaji wa aina hiyo kuanzia mabeki mpaka viungo,tunafurahia matunda yao yanaoenekana.

Huko Yanga kwa sasa huwaambii kitu na wala hawana maswali tena juu ya suala la ufungaji mabao ndani ya timu hiyo kutokana na viungo wao matata ambao kwa sasa wanatupia mabao ya maana.   Ndani ya Yanga kwa sasa vinara wa upachikaji mabao unashikiliwa na viungo watatu ambao ni Pacome Zouzoua,Maxi Nzegeli na Aziz KI ambao wote kwa pamoja wamefunga mabao matatu katika michezo mitano ambayo Yanga imecheza mpaka sasa.   Sasa kitendo hiko cha viungo hao wa Yanga kufunga mabao yakutosha kimemkuna kocha mkuu Miguel Gamond ambaye anaamini viungo hao watampa mabao ya kutosha na kuwakabidhi jukumu la kuhakikisha wanafunga mabao mengi Zaidi.   “Tunafurahi kuona tuna timu yenye wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao,ukiwa kama kocha lazima ikuvutie kwa kuwa unakuwa na uhakika kuwa utapata mabao mengi.   “Kwa upande mwingine inakuwa nzuri kwa kuwa kuna siku mbaya kazini kutoka kwa washambuliaji basi wao wanakuwa ni msaada mwingine tosha,naamini kwetu Yanga tumejaliwa wachezaji wa aina hiyo kuanzia mabeki mpaka viungo,tunafurahia matunda yao yanaoenekana. "Nimewaambia wanatakiwa kufunga katika kila nafasi itayopatikana,naamini wanafanyia kazi na matunda yanaonekana kwa kuwa wanafunga zaidi”alisema Gamondi.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live