Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome: Ilikuwa kama muujiza kuwafunga Belouizdad

Pacome Yanga Cr Pacome: Ilikuwa kama muujiza kuwafunga Belouizdad

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua amesema kuwa ilikuwa kama muujiza kuwafunga CR Belouizdad bao 4-0 kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumamosi iliyopita Februari 24, 2024 katika Dimba la Mkapa na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiy.

Pacome amesema kuwa kilichowasaidia ni mbinu za mwalimu Miguel Gamondi na kwamba yeye aliumia siku moja kabla ya mchezo uliopewa jina lake 'Pacome Day', jambo lililomhuzunisha lakini alidhamiria mchezo huo lazima acheze.

“Haikuwa rahisi sana kufuzu hasa ukizingatia mchezo wa kwanza tuliocheza ugenini dhidi ya CR Belouizdad tulipoteza, mchezo wetu wa juzi ni kama muujiza tu kuifunga Belouizdad. Maandalizi ya mwalimu ndiyo yalitusaidia sisi kupata matokeo chanya.

“Niliumia siku moja kabla ya mchezo, niliumia sana hasa nikiwaza Ofisa habari alikuwa amefanya kazi kubwa ya kuwaita mashabiki na wananchama na kikubwa zaidi ilikuwa siku yangu maalum. Nikiwaangalia wachezaji wenzangu roho yangu ilikuwa ikiniuma sana, sikuwa na jinsi zaidi ya kujikaza na kujipa moyo kwamba nitacheza.

“Nilimtanguliza Mungu na kulipokucha nikwaambia viongozi kwamba niko vizuri sana ninaweza kuendelea na mchezo uliofuata, ninamshukuru Mungu niliamka vizuri na kilichobaki ni historia na wote tulikishuhudia.

“Tunaelekea Misri kucheza na Al Ahly sio tu kwa ajili ya kuhitimisha mashindano bali kutafuta nafasi ya kwanza ili kukamilisha kundi, tunaamini tutafanikiwa” amesema Pacome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: