Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome, Hausung Vita ni vita

Pacome X Aziz Ki Majeruhi.png Pacome, Hausung Vita ni vita

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya mashabiki wa Yanga kukaa muda mrefu bila kuiona ikicheza tangu ilipotolewa kwenye Kombe la Mapinduzi, Januari 7, leo itarejea uwanjani katika mechi ya hatua ya 64 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Hausung FC, ambao ni mabingwa wa mkoa wa Njombe.

Mchezo huo ambao pia ni kiporo, utapigwa kuanzia saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Azam Complex, huku Hausung wakikomaa na Pacome Zouzoua asiwaletee madhara.

Katika mechi hiyo Yanga itaingia bila wachezaji saba ambao ni Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ Mudathir Yahya na Keneddy Musonda waliopewa mapumziko mafupi baada ya fainali za Afcon 2023, sambamba na Stephane Aziz Ki na Djigui Diarra ambao leo watakuwa uwanjani wakichuana katika hatua ya 16 bora, mechi zitakazokutanisha mataifa yao ambapo Diarra atakuwa na Mali huku Ki akiwa na Burkina Faso.

Akizungumza na Mwanaspoti kuhusu mchezo huo, kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alisema: “Ni mechi muhimu na tunataka kushinda ili kusonga mbele. Yanga ina wachezaji wengi na tutatumia zaidi tuliokuwa nao mazoezini katika siku za hivi karibuni na naamini tutashinda na kuwafurahisha mashabiki wetu.”

Kocha mkuu wa Hausung alisema Shangwe Michael alisema wanaiheshimu Yanga na watacheza kwa tahadhari kubwa na wamewafanyia kazi mastaa wote wa Yanga haswa Pacome ambaye wanajua staili yake ya uchezaji.

“Tutacheza kwa kuwaheshimu na lengo ni kushinda kwani hatua hii ni ya mtoano usiposhinda unatolewa,” alisema. Ukiachana na mechi hiyo ya Yanga na Hausung, katika uwanja wa Manungu, Turiani leo kutakuwa na mtanange mwingine wa ASFC ambapo Mtibwa itakuwa ikiikabiri Nyakagwe FC utoka Geita mechi itakayopigwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Kocha mkuu wa Mtibwa, Zuberi Katwila alisema atatumia mechi hiyo kufanya tathimini ya kikosi baada ya dirisha dogo la usajili huku lengo ni ushindi.

“Pamoja na kutafuta usahindi pia tutautumia kufanya tathmini ya kikosi chetu baada ya usajili tulioufanya na wachezaji wengi wapya watapata nafasi,”alisema

Mechi nyingine za ASFC zitapigwa kesho ambapo Simba itaikaribisha Tembo FC inayoshiriki Ligi ya Mkoa wa Tabora na Kagera Sugar itapepetana na Dar City.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: