Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome Aucho kuwakosa Mamelodi kesho

Pacomeeee Auchooo Pacome Aucho kuwakosa Mamelodi kesho

Fri, 29 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema atawakosa nyota wake wasiopungua watatu kwenye mchezo wa kesho robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Gamondi amesema wachezaji Khalid Aucho, Kouassi Attohoula, Pacome Zouzoua na Kibwana Shomari bado hawajawa na utimamu wa kimwili hivyo huenda akawakosa kwenye mchezo huo.

“Natarajia kuwakosa baadhi ya wachezaji wangu nyota, siwezi kuhatarisha afya za wachezaji ambao bado hawana utimamu wa kimwili. Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kukosa wachezaji watatu mpaka wanne" amesema Gamondi alipokuwa akizungumzia maandilizi kuelekea mchezo huo.

Mchezo huo utapigwa kesho saa tatu usiku Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.

Una maoni, tuandikie.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live