Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacome, Aucho, Yao warejesha tabasam la Wananchi

Pacomeeee Auchooo Pacome, Aucho, Yao warejesha tabasam la Wananchi

Mon, 1 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kurejea kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu akiwemo Pacome Zouzoua ambao walikuwa majeruhi, umempa jeuri kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ambaye anaamini kuwa wanaweza kwenda Afrika Kusini na kufanya vizuri katika mchezo wa robo fainali ya pili, Ijumaa ijayo ya Aprili 5 dhidi ya Mamelodi Sundowns F.C.

Yanga ikiwa katika kiwango bora bila ya Pacome, Khalid Aucho na Kouassi Attohoula Yao, ilitoka suluhu juzi, Jumamosi katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Hivyo wanahitaji ushindi au japo sare ya mabao yoyote katika mchezo wa marudiano ili kutinga hatua ya nusu fainali.

“Siwadai wachezaji wangu hakika wamecheza vyema na kufuata maelekezo, tumekutana na timu kubwa na bora ambayo ina uzoefu na hii michuano, ukiwa mwalimu na wachezaji wakawa wanacheza kwa kufuata maelekezo yako basi unafurahia na ndio furaha niliyoipata hata kama hatujapata ushindi,”

“Kwa sasa tunaenda ugenini tukiwa na matumaini ya wachezaji wengine ambao walikosekana kutokana na kuwa majeruhi kurejea na ukweli ni kwamba natamani tucheze fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.”

Katika mchezo huo, Gamondi ameonyesha kuwa yeye ni aina ya makocha ambao wanaweza kubadilika muda wowote kulingana na mazingira kiasi cha kumpa wakati mgumu kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena ambaye alikiri hilo.

Gamondi aliamua kuingia na mabeki wa tatu wa kati ambao ni Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na Dickson Job ambaye alicheza kulia ambako Yao na Kibwana Shomary ni majeruhi, huku katika eneo la kati ambalo alizoeka kucheza Aucho alimtumia Jonas Mkude na mbele akaanza na washambuliaji wawili.

Yanga ilikuwa bora katika kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza kupitia maeneo yote ya uwanja huku pasi za kuchana ukuta za Stephane Aziz Ki na Mudathir Yahya zingeweza kuipa ushindi mzuri Yanga kama zingetumiwa vyema na washambuliaji wao,

Sasa taarifa kutoka ndani ya Uongozi wa klab hiyo ni kuwa Wachezaji hao 3

????️Pacome ????️Yao ????️Aucho

Watakuwepo kwenye mchezo wa marudiano huko Afrika kusini dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Yanga wanahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili waweze kusomba mbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live