Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacha wa Neymar azua gumzo

Neymarv Pacha wa Neymar azua gumzo

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Neymar alikuwa anakaribia kurejea katika Kombe la Dunia, mwingine alikuwa akirejea nyumbani baada ya kukaa kwa muda mfupi - na kuzua hisia tofauti - huko Qatar.

Kulingana na jarida la SportStar , Neymar halisi amepona jeraha la kifundo cha mguu na alishiriki katika mechi ya Jumatatu dhidi ya Korea Kusini katika hatua ya 16 bora, huku mwonekano wake nchini humo ukizua msisimuko mkubwa

Eigon Oliveira, ambaye anajiita "Ney's Lookalike," alikuwa na shughuli nyingi katika ziara yake huko Qatar, ambapo alivutia umakini mwingi akionekana kama Neymar.

Sportstar inadai kwamba Ilikuwa vigumu kubaini tofauti kati ya Neymar halisi wakati Oliveira alipovaa sare ya mazoezi ya Brazil na kuvaa miwani ya jua, kofia na ndevu sawa na nyota huyo wa Brazil.

Pia alionekana kuwa na tattoos sawa na Neymar, na kwa kawaida aliandamana na rafiki ambaye alivalia kama mfanyikazi wa shirikisho la kandanda la Brazil. Baadhi ya marafiki zake pia mara nyingi walijifanya kama walinzi wake.

Duka la Puma mjini Doha lililazimika kufungwa kwa muda wakati Oliveira alipotembelea na kuvutia mamia ya mashabiki. Ilibidi apelekwe nyuma ya duka hadi mambo yatakapotulia.

Kulikuwa na hali ya mshikemshike wakati mtu huyo anayefanana na Neymar alipoingia kuhudhuri mojawapo ya mechi ya kombe la Dunia ya Brazil , huku mashabiki wakipiga kelele wakitaka kupiga picha naye.

Baadhi ya wachezaji wa Brazil waliokuwa uwanjani kabla ya mechi kumalizika walitazama juu kuona kinachoendelea. Hatahivyo maafisa wa usalama baadaye walimuondoa mtu huyo na kumsindikiza .

Kabla ya mechi moja, Oliveira alifanikiwa kufika uwanjani huku baadhi ya walinzi wakidhania kuwa alikuwa Neymar halisi

Kwa mujibu wa Sportstar , Oliveira ana wafuasi milioni 1 kwenye Instagram na yuko karibu na alama hiyo hiyo kwenye TikTok. Anarekodi vituko vyake vingi na kuzichapisha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii, ambapo zinasambaa kwa kasi.



Kuwa mtu anayefanana na Neymar kumemaptia kazi bwana Oliveira. Amezunguka dunia nzima akimuiga mchezaji huyo, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, ambapo Neymar anakipiga katika klabu ya Paris Saint-Germain.

Anatengeneza pesa kutokana na mwonekano wake na kwa kuigiza kama mtu anayefanana na nyota huyo wa Brazil hata pia katika matangazo ya biashara.

Aliviambia vyombo vya habari vya Brazil kwamba yote yalianza alipokuwa akifanya kazi kama mhudumu katika mgahawa mmoja huko Brazil na watu walianza kuzungumza kuhusu kufanana kwake na Neymar halisi, hatua ambayo ilimfanya kuajiriwa na wakala.

Amekutana na Neymar mara chache katika baadhi ya filamu zake za kibiashara, na akasema kwamba ni sawa kwa jamaa huyo kuendelea kujifanananisha nay eye.

"Sijawahi kufikiria wakati huu," alisema katika chapisho la hivi karibuni. Nimebarikiwa kufika mbali na kazi hii. Ninashukuru sana na mimi ni shabiki wa kijana huyu ambaye anakumbatia ninachofanya kwa mikono miwili.

"Alibadilisha maisha yangu kwa njia kubwa, akinipa mamilioni ya majukumu na fursa, na kuniruhusu kwenda mahali na kukutana na watu ambao sikuwahi kufikiria kwenda au kukutana nao.

Oliveira alisema ana mpango wa kurejea Qatar kwa nusu fainali ikiwa Brazil itasonga mbele, kwa hivyo kunaweza kuwa na msisimuko mwengine utakaosababishwa na mtu huyo anayefanana na nyota w Brazil Neymar kabla ya Kombe la Dunia kumalizika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live