Kocha wa Simba, Pablo Franco huwa hazoezeleki maana kila mchezo huwa anakuja na sapraizi mpya kwa mashabiki.
Kikosi alichoanzisha leo dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) uwanja wa Benjamin Mkapa, kamuanzisha benchi golikipa namba moja Aishi Manula.
Kukosekana kwa Manula kumetoa nafasi kwa kipa namba mbili Beno Kakolanya kuanza kwenye eneo hilo ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuweza kucheza kwa msimu huu.
Kwa upande wa winga Peter Banda anaanza baada ya kukosa mchezo uliopita na Yanga.
Mara ya mwisho kwa Banda kuanza ilikuwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold uliofanyika Desemba Mosi alipofunga bao moja na kuisaidia timu yake kushinda mabao 2-1.
Kikosi kamili kinachanza kwenye mchezo huo ni Beno Kakolanya, Israel Mwenda, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Sadio Kanoute, Peter Banda, Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Pape Osmane Sakho na Yusuph Mhilu.
Wachezaji wa akiba ni Ally Salum, Shomari Kapombe, Henock Inonga, Jonas Mkude, Abdulswamad Kassim, Duncan Nyoni, Meddie Kagere, Ibrahim Ajib na Jimmyson Mwanuke.
Simba inashuka uwanjani usiku huu wakiwa ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo.