Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo azuiwa kwa muda kuingia uwanjani

Pablo Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco Martin

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Shamra shamra za hapa na pale, zinaendelea nje ya Uwanja wa Manungu, ambako saa 10:00 jioni inapigwa mechi ya wenyeji Mtibwa Sugar na Simba.

Kama ilivyo ada penye umati wa watu hapawezi kukosekana vurugu za hapa na pale ndio hali halisi inayoendelea nje ya uwanja huo.

Mashabiki wanalalama kuzuiwa kuingia uwanja baada ya kufika mapema wakidai tiketi walikata mapema,lakini hawaelewi kwa nini wanawekewa kipingamizi.

Jambo ambalo linawalazimu askari kutuliza vurugu kwa njia ya amani na kuwataka mashabiki hao kuwa na subra, hadi watakaporuhusiwa.

Ni kama kadhia hiyo imemkumba na kocha wa Simba, Pablo Franco ambaye alionekana kusimama takribani dakika 4 akisubiria kuingia kukagua uwanja, jambo ambalo lilifanya mabaunsa wa timu hiyo kupaniki.

Jambo lililozidi kuchochea kelele za mashabiki kuona anazuiwa kocha wao kwa ajili ya uwanja kujaa maji, lakini bado askari walizidi kuwatuliza bila kutumia nguvu.

Hata hivyo Mwanaspoti limeingia ndani ya uwanja kuangalia hali halisi ya uwanja ambapo pembeni ya uwanja kunaonekana kuna ubichi ubichi, wakati pichi kuna watu wanaonekana kuchota maji na kwenda kuyamwaga nje.

Chanzo: Mwanaspoti