Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo aachiwa msala Simba

PAblo MKapa St Pablo Franco Martin

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: Mwananchi

Simba inatarajiwa kushuka uwanjani leo mjini Tabora kuvaana na KMC, huku kocha mkuu wake, Pablo Franco akiachiwa msala juu ya hatma ya nyota wapya wanaowindwa ili kujiunga na timu hiyo kupitia dirisha dogo.

Tayari mezani mwa mabosi wa Simba kuna majina mawili likiwemo la winga Harrison Mwendwa kutoka Kenya na straika Alex Bazo wa Nkana FC ya Zambia, lakini uongozi huo umekataa kujivisha mabomu kwa kuwasainisha kabla hawajajadiliana na kocha wao.

Habari za ndani zilizothibitishwa na mmoja wa vigogo wa klabu hiyo ni kwamba, wamepanga kufanya kikao maalumu pamoja na Kocha Pablo, Jumatatu ijayo ili kujadiliana juu ya usajili wa nyota wapya wanaotakiwa kusajiliwa kwenye dirisha hili.

“Tunasubiri timu irejee kutoka Tabora na Desemba 27 tutakaa pamoja ili kuwekana sawa na kupitisha wanaofaa kusajiliwa. Tunafanya hivi ili kuepuka lawama kama ilivyotokea baada ya wachezaji waliosajiliwa kwa sauti ya mtu mmoja, kushindwa kuwapa matokeo chanjya,” alisema kigogo huyo aliyeomba asitajwe jina gazetini.

Kigogo huyo alifafanua, kocha Pablo alishawapa ripoti yake ikipendekeza wachezaji wa kupigwa chini na wale anaowataka wasajiliwe na wanalitekeleza, ila uamuzi wa mwisho wa sajili hizo mpya utabaki mikononi mwa kocha.

“Hatutaki lawama, mbali na nyota hao wawili wa kigeni, pia kuna wachezaji wawili wa kizawa akiwamo kipa tunaendelea kuwafuatilia na wote watajadiliwa kwa kumsikilizia kocha ataamua vipi,” alifafanua.

Msimu uliopita kwenye dirisha dogo, Simba ikiwa chini ya Didier Gomes, walisajiliwa wachezaji wapya wasiopungua wanne, lakini ni mmoja tu tu waliosalia kikosini kwa uwezo wake uwanjani naye ni Taddeo Lwanga, huku Peter Maduhwa, Lokosa Junior na Perfect Chikwenda walichemka.

Chanzo: Mwananchi