Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo: Tumewasisitiza wachezaji kutumia nafasi

Pablo Martin 5 3 22 Pablo Franco Martin

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa wekundu wa Msimbazi, Pablo Franco Martin amesema amewasisitiza wachezaji wake kuhakikisha wanatumia vyema nafasi wanazotengeneza kwenye michezo yao ili kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Dodoma Jiji.

Pablo amesema Benchi la ufundi linaendelea kuhakikisha wanatoa maelekezo vyema ili kutumia nafasi na kupunguza presha na kucheza soka lao la kawaida la kuburudisha mashabiki maarufu kiama pira biriani.

"Tumewasisitiza wachezaji kuhakikisha wanatumia kila nafasi wanayopata ili kujipunguzia presha na kucheza soka letu tulilolizoea.

Tunajua mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga kucheza vizuri na kuibuka na alama tatu, tutawatumia wachezaji ambao watakuwa tayari kimwili na kiakili " amesema Pablo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live