Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pablo : Nimefurahi kufuzu, tumestahili

Pablo Franco Martin Winner Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco Martin

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Pablo Franco, amesema amefurahi timu kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwani ndiyo yalikuwa malengo ya timu.

Pablo amesema waliingia na mbinu za kuhakikisha hawawapi nafasi ya kufunga mapema kwani wangewatoa mchezoni kitu ambacho walikimudu hadi dakika 10 za mwisho kuelekea mapumziko.

Pablo akizungumzia mchezo huo amesema waliwapa Red Arrows nafasi ya kumiliki mpira na kushambulia kwa kushtukiza ili kupata bao la mapema ambalo lingewawatoa mchezoni kwa kuwa walikuwa na mtaji mzuri wa mabao.

“Tulitaka kutafuta bao la mapema ambalo lingewachanganya wapinzani, mwanzoni tulipata nafasi mbili kubwa zile za Hassan Dilunga ambazo kama tungefunga tungemaliza mechi mapema.

“Lakini nimefurahi kwa matokeo haya kwa kuwa malengo yetu yalikuwa kufuzu hatua ya makundi na tumefanikiwa, tunajua mashindano haya ni magumu kadri unavyosonga mbele lakini tutajipanga ili kuendelea kufanya vizuri,” amesema Pablo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live