KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco raia wa Hispania, amefunguka kuwa anaamini ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu hauna mwenyewe, licha ya wapinzani wao Yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano.
Pablo ametoa kauli hiyo baada ya juzi Jumapili Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza na kufikisha pointi 31 ikiwa ni tofauti ya pointi tano dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Yanga wenye pointi 36.
Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema kupata matokeo hayo ya ushindi kumerudisha hali ya kuendelea kufanya vizuri katika mechi za ligi licha ya kukiri kuwa bado suala la ubingwa mpaka sasa halina mwenyewe kutokana na ushindani ulivyo.