Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG yashinda ugenini, Neymar apata majeraha, Messi usipime

Neymar Neymar akiugulia maumivu

Sun, 28 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la Paris wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Saint-Etienne katika dimba la Stade Geoffroy Guichard.

Magoli ya PSG katika mchezo huo yamefungwa na Marquinhos aliefunga magoli mawili na Angel Di Maria akifunga goli moja lakini mtengenezaji wa magoloi yote hayo akiwa ni Lionel Messi.

Katika mchezo huo, winga wa PSG, Neymar alilazimika kutolewa nje kwa machela baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu.

Neymar alipigwa picha akiondoka uwanjani kwa magongo na huku akitumai fowadi huyo atapona haraka, Pochettino alieleza kuwa PSG lazima isubiri uchunguzi kamili Jumatatu.

“Hakuna la kusema zaidi kwa sasa, ni maumivu aliyoyasikia kwenye mguu na kifundo cha mguu. Tutafanya vipimo kesho na tutaona,” Pochettino aliambia mkutano wa wanahabari.

Hapo awali Pochettino aliiambia Amazon Prime: “Tutalazimika kuona hii kesho lakini kutokana na picha, ninatumai kwamba sio jambo kubwa na atarejea na kikosi haraka. Lakini hatua si nzuri.”

Baadaye Neymar alichapisha taarifa kwenye akaunti yake rasmi ya Instagram.

“Vikwazo hivi ni sehemu ya maisha ya mwanamichezo,” aliandika. “Sasa hiyo ndiyo uliyo nayo, inua kichwa chako twende. Nitarudi nikiwa na nguvu zaidi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live