Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG yashinda 4, Ramos akiingia kambani

Sergio Scored Ramos akishangilia goli usiku wa jana

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la Paris, Paris St-Germain wameibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Reims katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1 mtanange uliopigwa dimba la Parc des Princes.

Katika ushindi huo mlinzi wa kati wa zamani wa Real Madrid Sergio Ramos alifunga bao moja na kuandikisha bao lake la kwanza katika uzi wa PSG.

Magoli mengine ambayo yamefungwa kwenye ushindi huo ni ya Marco Verratti likiwa bao lake la kwanza tangia mwaka 2017, Wout Faes akajifunga na bao la mwisho limefungwa na Danilo kwa shuti la mguu wa kushoto.

Matokeo hayo yanaifanya PSG kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya timu iliyo nafasi ya pili Nice.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live