Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG yamkazia Mbappe" Utasaini au usepe"

Mbappe Nahodha Mpya Ufaransa Amrithi Lloris Kylian Mbappe

Sun, 25 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo ni moto. Na lisemwalo ni kwamba Paris Saint-Germain imemwambia Kylian Mbappe anapaswa kuchagua moja, ama asaini mkataba mpya wa kubaki Parc des Princes au auzwe.

Fowadi huyo supastaa wa kimataifa wa Ufaransa ndani ya mwezi huu waliwashtusha mabosi wa klabu ya PSG baada ya kuwaambia kwamba hana dhamira wala mpango wa kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho kwa zaidi ya mwaka 2024.

Mbappe mkataba wake huko PSG, unaoripotiwa kuwa na thamani ya Pauni 500 milioni, utafika tamati 2024 - lakini una kipengele kinachoruhusu kubaki hapo hadi 2025 kama atakubali kukifanyia kazi kipengele hicho.

Mwaka wa ziada kwenye mkataba huo wa Mbappe ni uamuzi wa mchezaji, hivyo kama mkali huyo wa Ufaransa atataka kukifanyisha kazi kipengele hicho au la.

Mbappe, 24, alituma barua maalumu kwa mabosi wa PSG kuwaambia kwamba hakuna kitakachomfanya akifanyishe kazi kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake cha kuendelea kubaki hapo hadi 2025.

PSG awali ilisisitiza kwamba haimtarajii Mbappe kuondoka Parc des Princes kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi huko Ulaya na mchezaji mwenyewe yupo tayari kubaki kwenye timu hiyo kwa sasa, walau kwa mwaka wa mwisho wa kimsingi katika mkataba wake, awepo Parc des Princes hadi 2024.

Lakini, sasa mabosi wa PSG wamebadili mawazo, wanataka kumpiga bei Mbappe kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ili wapate chochote kitu kuliko kumpoteza bure mwakani.

Real Madrid wamekuwa wakimpigia hesabu mshambuliaji huyo kwa muda mrefu sana na rais wa miamba hiyo ya Bernabeu, Florentino Perez alihitaji kunasa saini yake na kuikosa miezi 12 iliyopita.

Na sasa, biashara ya usajili ya Real Madrid kwenye dirisha hili inaripotiwa kukamilika baada ya kumsajili straika veterani, Joselu kwa mkopo huku ikitumia Pauni 115 milioni kunasa saini ya kiungo Jude Bellingham.

Perez anasubiri hadi dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi 2024 ili kupata saini ya mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018, ambapo atakuwa anapatikana bure sokoni. Lakini, shida PSG hawataki kufanya huo uzembe wa kubaki na Mbappe hadi mwakani wakati wanafahamu wazi hatasaini dili jipya na wao wataingia hasara ya kumpoteza bure kabisa mchezaji ambaye angewaingizia pesa ya kutosha.

Na sasa imemwambia mchezaji huyo aamue moja, kusaini mkataba mpya au apigwe bei. Na kwenye hilo, Manchester United imeelezwa nayo kuhitaji saini ya Mbappe.

Na huenda akaweka mezani ofa ya kubadilishana wachezaji mara tu tajiri wa Qatar, Sheikh Jassim atakapokamilisha mchakato wa kuinunua klabu hiyo. Kutokea kwenye kambi ya PSG ni kwamba wamiliki wa klabu hiyo wenye maskani yao Doha, Qatar wapo tayari kumuuza mchezaji huyo na huenda watakuwa kwenye furaha kubwa kufanya biashara na Man United endapo kama itakuwa chini ya ndugu yao wa Qatar, Sheikh Jassim.

PSG kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kukamilisha kumtangaza Luis Enrique kuwa kocha wao mpya na imempa Mbappe, ambaye kwa sasa yupo likizo baada ya kukamilisha majukumu ya timu ya taifa ya Ufaransa na baada ya wiki mbili au tatu awe ametuliza akili yake na kufanya uamuzi, anasaini dili jipya au auzwe.

PSG haijafunga milango ya kumuuza Mbappe huko Real Madrid, lakini hawatafanya hivyo kwa bei ndogo. Kinachoelezwa ni kwamba miamba hiyo ya Paris haitakubali mkwanja usiozidi Pauni 172 milioni kwenye mauzo ya mshambuliaji huyo wa zamani wa AS Monaco.

Taarifa zaidi zinafichua kwamba PSG haitampigia magoti mchezaji yeyote kwa sasa huku wamiliki wake wakitaka kuifanya klabu kubwa kubwa kuliko kitu kingine chochote na sasa kila kitu kipo kwa Mbappe, kuamua atasaini mkataba mpya au klabu impige bei dirisha hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live