Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG yakwama Ligue 1, yachapwa 2 na Rennes

Rennes 2 PSG 0 Lionel Messi Brought Back To Earth With A Bump As PSG Suffer Shock Loss Days After Ta PSG vs Rennes

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la Paris klabu ya PSG, siku ya Jumapili hawakuamini kilichowatokea mbele ya Rennes baada ya kukamilisha dakika 90 pasipo kulenga hata shuti moja golini.

PSG ambayo ilianza na nyota wake wote watatu tishio barani ulaya na duniani, Kylian Mbappe, Neymar, Angel Di Maria na Lionel Messi ilishuhudia ikichapwa magoli 2-0.

Rennes walifanya kazi ya ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote katika safu yao ya ulinzi na muda mwingi wa mchezo walikua wakikaba pamoja.

Magoli ya Rennes yamefungwa na Gaetan Laborde 45' na Flavien Tait 46' na kuihakikishia ushindi Rennes.

Matokeo hayo yaliyoshangaza wengi yameanza kuleta picha mbaya kwa kocha wa Kikosi hicho Mauricio Pochettino na wengi kumuona kama ataonyeshwa mlango wa kutokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live