Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG yajiandaa kumtwaa Osimhen

Maxresdefault 5 PSG yajiandaa kumtwaa Osimhen

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Imefahamika kuwa Mabosi wa Klabu Bingwa nchini Ufaransa Paris-Saint Germain wanahaha kumtafuta mbadala wa Kylian Mbappe ambaye ameshawataarifu kwamba ataondoka mwisho wa msimu huu kama mchezaji huru.

Kwa sasa mabosi hao wanafikiria kumshusha nyota wa kimataifa wa Nigeria na SSC Napoli ya Italia Victor Osimhen, na wanaona nyota huyo ambaye mkataba wake na mabingwa hao wa Serie A utamalizika mwaka 2026, atawafaa zaidi.

Awali, PSG ilikuwa ikipambana kuona itafanya nini ili Mbappe asiondoke bure na angeongeza mkataba mpya utakaoipa faida kutokana na mauzo yake. Hata hivyo kwa sasa haitanufaika naye kwani anaondoka bure.

Osimhen mwenye umri wa miaka 25, alionyesha kiwango bora msimu uliopita akiwa na SSC Napoli na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya ltalia na akiibuka pia mfungaji bora wa ligi.

Hata hivyo, inaonekana ni vigumu kumpata kwa urahisi kwa kuwa SSC Napoli inahitaji zaidi ya Euro 100 milioni na kuna utitiri wa timu nyingi zinazopambana kumsajili.

Chanzo: Dar24