Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG yaingia vitani kuiwinda saini ya Nico Williams

Nico Williams Nico Williams

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Paris St-Germain imeingia katika vita ya kuiwaia saini ya staa wa Athletic Bilbao, Nico Williams katika dirisha hili ambapo inaumana na Chelsea na Arsenal ambazo ndio za kwanza kuonyesha nia ya kumsajili fundi huyu wa kimataifa wa Hispania ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

Msimu uliopita alicheza mechi 38 za michuano yote, amefunga mabao manane na kutoa asisti 19.

GOLIKIPA wa akiba wa Liverpool, Adrian, 37, yupo katika hatua za mwisho kujiunga na Real Sociedad katika dirisha hili ambako anaweza kwenda kustaafia.

Kipa huyu wa kimataifa wa Hispania mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu na msimu uliopita hakucheza mechi hata moja katika kikosi hicho cha Majogoo wa Anfield.

CHELSEA imemuongeza katika orodha ya washambuliaji inaohitaji kuwasajili katika dirisha hili staa wa Hoffenheim, Maximilian Beier, 21, ambaye msimu uliopita alionyesha kiwango bora akifunga mabao 16, katika mechi 36 za michuano yote.

Beier ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2027. amewavutia mabosi wa Chelsea kutokana na umri wake na moto anaowasha.

NEWCASTLE United inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa AC Milan katika harakati zao za kumsajili straika wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 27, katika dirisha hili.

Lewin anaonekana kuwa mshambuliaji sahihi wa kwenda kuziba pengo la Olivier Giroud aliyeondoka Milan, mwisho wa msimu uliopita.

OLYMPIQUE Lyon imeingia katika vita na baadhi ya timu nyingine kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa Newcastle United na Gambia, Yankuba Minteh, 19, ambaye pia anawindwa na Everton.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za usajili, Fabrizio Romano, staa huyu tayari ameshafanya makubaliano na moja kati ya timu zinazotajwa.

NOTTINGHAM Forest imeanza mazungumzo na Aston Villa kwa ajili ya kumsajili beki wa timu hiyo na Uholanzi, Lamare Bogarde, 20, katika dirisha hili.

Borgade ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Bristol Rovers, alicheza jumla ya mechi 27 za michuano yote na kutoa asisti mbili. Mkataba wake unamalizika mwaka 2025.

BORUSSIA Dortmund ipo katika hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Brighton, Pascal Gross, 33, katika dirisha hili kwa dau linalodaiwa kuwa kati ya Euro 7 hadi 10 milioni.

Gross ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Brighton, mkataba wake wa sasa unararajiwa kumalizika mwakani.

Chanzo: Mwanaspoti