Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG yachezea Kichapo Ligue 1

Paris Vs Monaco H Monaco imeibuka na ushindi wa Magoli 3-0

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paris St-Germain imekutana na kipigo kizito kwa mara ya kwanza tangia msimu wa 2019 baada ya jana Jumapili kufungwa bao 3-0 dhidi ya Monaco katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1.

Wakiwa nje ya kiwango chao, PSG imefungwa magoli hayo na kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Ufaransa huku kocha Mauricio Pochettino akikalia kuti kavu.

Katika mtanange huo, mabao yamefungwa na Wissam Ben Yedder aliyefunga goli mbili na Kevin Voland aliyetumia pasi ya Yedder.

Kinakuwa ni kichapo cha nne katika mechi sita zilizopita kwenye mashindano yote yaliyopita.

Akizungumzia mchezo huo, Pochettino amesema “Namna ambavyo tumepoteza haikubaliki”.

“Hatuwezi kuanza mchezo kama ambavyo tulianza”, aliongeza Pochettino. “Tunatakiwa kusahau kuwa tumepoteza Ligi ya Mabingwa na kufikiria kufanya vizuri sehemu nyingine”.

Kwa matokeo hayo, Pochettino ataendelea kuwa kwenye presha kubwa ya kuondoka klabuni hapo kutokana na kuhusishwa na klabu ya Manchester United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live