Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG wanamtaka Haaland

Haaland Dsmf PSG wanamtaka Haaland

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo wa Ufaransa, Paris Saint-Germain wanataka kufanya usajili wa kutisha ndani ya kikosi hicho, baada ya kutenga fungu nene kwa ajili ya kumsajili straika straika, Erling Haaland wa Manchester City.

Vigogo hao wametenga kiasi cha euro milioni 175 kwa ajili ya kumsajili Haaland ambaye amekuwa na msimu mzuri tangu atue Man City akitokea Dortmund mwanzoni mwa msimu huu akifunga mabao 28 mpaka sasa kwenye Premier.

PSG wanataka kumleta Haaland ndani ya kikosi chao kwa ajili ya kuungana na kinda mwenzake, Kylian Mbappe na kuifanya timu hiyo itemize ndoto yake ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’ ambalo wamekuwa wakilitamani kulibeba, ambapo msimu huu wameondolewa na Bayern kwenye hatua ya 16 Bora.

Kwa mujibu wa mwandishi, Daniel Riolo, PSG wanataka kuitengeneza pacha ya Haaland na Mbappe ambayo wanaamini itakuwa na manufaa ndani ya kikosi hicho.

Riolo anaongeza kuwa ujio wa Haaland ndani ya PSG utatokana kwa kuwa timu hiyo inaweza kuwauza mastaa wake, Neymar na Lionel Messi, mwishoni mwa msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live