Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG wamgeukia Barnado Silva

Bernado Silva Bernad Bernado Silva

Wed, 17 May 2023 Chanzo: Dar 24

Uongozi wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa PSG unataka kuhakikisha unamsajili Kiungo Mshambuliaji wa Manchester City Bernardo Silva, wakati wa usajili wa majira ya Kiangazi, ili akawe mbadala wa Lionel Messi ambaye ataondoka mwisho wa msimu baada ya mkataba wake kumalizika.

Silva mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akihusishwa sana kuondoka Man City na timu iliyokuwa ikitajwa huenda atajiunga nayo ilikuwa ni FC Barcelona.

Hata hivyo, kuingia kwa PSG kwenye dili hili kunakwenda kuzidisha upinzani ingawa moyo wa Silva unaonekana kuitamani zaidi Barca.

Hata hivyo, moja ya sababu zinazoipata nafasi ndogo FC Barcelona ni kwenye suala zima la masilahi na watatakiwa kuuza baadhi ya mastaa ili kupata pesa za kuvinja mkataba wa kiungo huyu.

Wakati huo huo, Barca pia inahusishwa na harakati za kutaka kumrudisha Messi, kutokana na bajeti yao na namna La Liga inavyowabana itakuwa ngumu sana kwao kuwachukua Silva na Messi kwa wakati mmoja.

Mkataba wa sasa wa Silva unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Msimu huu amecheza mechi 51 za michuano yote, amefunga mabao matano na kutoa asisti saba.

Chanzo: Dar 24