Wakati mustakabali wa Harry Kane katika kikosi cha Tottenham Hotspurs haujulikani, huku mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2024 na sasa kuna ripoti matajiri wa jiji la Paris, Paris Saint-Germain imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.
Kutokana na hali hiyo, uvumi unazidi kuibuka kuhusu kutakiwa kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England wakati wa dirisha la joto lijalo.
Manchester United wanajulikana kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, huku FC Bayern Munich pia hapo awali walihu- sishwa.
Na ripoti za hivi sasa zinesema Paris Saint-Germain wanawania kunasa saini ya mshambuliaji huyo, kwa mu- jibu wa gazeti la Le Pa- risien.
Mkurugenzi wa Michezo wa PSG, Luis Campos, anataka kuimarisha safu ya ushambuliaji na amemtambua Kane kama shabaha yao kuu.
Rais wa klabu hiyo ya Ufaransa, Nasser Al Khelaifi, ana uhusiano mzuri na Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, jambo ambalo linaweza kusaidia mazungumzo.