Paris Saint-Germain wako tayari kutumia kitita cha euro milioni 140 kupata huduma za nyota wa Arsenal mwenye umri wa miaka 22 Bukayo Saka.
Fichajes anaripoti kuwa Paris Saint-Germain wanajiandaa kwa dirisha la kihistoria la uhamisho wa majira ya kiangazi ambapo wanataka kumsajili Saka.
Mabingwa hao wa Ufaransa wanatafuta mshambuliaji bora zaidi ili kuimarisha kikosi cha Luis Enrique, kwa sababu Kylian Mbappe ataondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu.
Mkataba wa Mbappe unaisha msimu utakapokamilika. Mchezaji huyo tayari amefanya chaguo kuhusu mustakabali wake, hata kama PSG wangetaka kubaki naye kwa muda mrefu zaidi. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ameamua kuhamia Real Madrid na hana mpango wa kubaki katika klabu hiyo ya Ufaransa.