Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG waingia matatani sakata la mauzo ya Mastaa hawa..!

Marco Verratti PSG waingia matatani sakata la mauzo ya Mastaa hawa..!

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) linapanga kuchunguza hamisho za wachezaji watatu wa PSG, Marco Verratti, Abdou Diallo na Julian Draxler kwenda vilabu vya Qatar, Nchi ambayo ni mwanahisa mkuu wa klabu hiyo ya Ufaransa kupitia mfuko wake wa uwekezaji Qatar Sports Investments.

PSG imekusanya kiasi cha Euro milioni 80 kwa mauzo ya Verratti (€45M) Diallo (€15M) na Draxler (€20M) kwenda Qatar hivyo UEFA itachunguza miamala hiyo mitatu kwa ajili ya kutoa hukumu ikiwa kuna uhusiano wa karibu kati ya wahusika.

PSG imetumia zaidi ya euro milioni 300 kwenye usajili kwenye majira haya ya kiangazi hivyo UEFA inahisi kuna janja janja zinatumika kati ya PSG na Qatar ambao ndio wamiliki wa klabu hiyo ili kukidhi mahitaji ya Financial Fair Play (FFP)

Ikiwa UEFA itabaini kuwa kuna mchezo wa aina hiyo basi PSG haitaruhusiwa kuingiza mauzo ya wachezaji hao kwenye akaunti zake hali ambayo itapelekea kukumbana na rungu la FFP.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live