Klabu’ ya PSG wamempa mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wao Kylian Mbappe ikiwa ni katika njia ya kumzuia asiondoke kwenye dirisha lijalo kujiunga na ‘klabu’ ya Real Madrid.
Kwa mujibu wa tovuti ya AS inaeleza kuwa mkataba huo wa miaka miwili ambao PSG wameuweka mezani unadaiwa kuwa na thamani ya Pauni 136 milioni ambazo ni mjumuisho wa mshahara na ‘bonasi’ ya usajili.
Mkataba wake wa kwanza mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na alikuwa na mpango wa kuondoka tangu mwanzo wa msimu huu lakini ilishindikana.
Hata hivyo Mbappe mwenye umri wa miaka 25, anadaiwa kuwa tayari ameshafanya uamuzi wa kuondoka PSG mwisho wa msimu na kuelekea Madrid, lakini ‘mabosi’ wa ‘klabu’ hiyo hawataki kukubaliana na hilo.