Wakati PSG ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuondoshwa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa kupoteza mabao 3-0 ya ujumla.
Kuna taarifa zinadai kuwa mmoja wa wachezaji walioanza katika mchezo wa mkondo wa pili alionesha tabia za ulevi siku mbili kabla ya mchezo huo lakini cha ajabu alipata nafasi ya kuanza.
"Kuna mchezaji wa PSG aliyeanzishwa katika kikosi cha kwanza dhidi ya Bayern kwenye Uwanja wa Allianz Arena ambaye alifika katika mazoezi ya Jumatatu akiwa amelewa, siku mbili kabla ya mechi hiyo,” amedai mwandishi wa habari Romain Molina akidai kocha Christophe Galtier alimuanzisha mchezaji huyo, ambaye amelificha jina lake.
Katika mechi hiyo PSG walikubali kichapo cha magoli 2-0, huku mchezo wa awali wakipokea kichapo cha goli 1-0.