Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG kuanza kutumia viwanja vipya vya mazoezi

D1ry74hm 720 PSG kuanza kutumia viwanja vipya vya mazoezi

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya PSG imefungua rasmi na kuonyesha kwa ndani viwanja vyake vipya vya mazoezi. Eneo hilo ambalo limechukua mwaka mmoja kujengwa lipo "Poissy" takribani kilomita 24 kutokea Paris.

Ndani ya eneo la viwanja hivyo kuna mabwaya ya kuogelea ya kifahari na zaidi ya vitanda 140.

Eneo la viwanja hivyo litakaloanza kutumiwa msimu huu limegharimu pauni milioni 257 kukamilika.

Baada ya kuondoka Camp des Loges mwezi Juni sasa mabingwa hao wa Ufaransa watahamia mahali hapa.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuhama viwanja vya mazoezi tangu klabu hiyo iundwe mwaka 1970.

Timu mbalimbali za klabu hiyo zitatumia eneo hilo zikiwemo timu za soka za wanawake na wanaume, timu za academy, timu ya mpira wa mikono pamoja na Judo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live