Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PSG hawana mpango na Ounahi

Azzedine Ounahi Azzedine Ounahi

Sat, 14 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya PSG mabingwa watetezi wa wa ligi kuu ya Ufaransa wameweka wazi hawana mpango na kiungo wa kimataifa wa Morocco Azzedine Ounahi anayekipiga Angers.

Klabu ya PSG chini ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Ocampos wameweka wazi hawana mpango wa kumsajili kiungo anayekipiga katka klabu ya Angers inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa pia. Zaidi wanawekeza kwenye vijana walioko ndani ya klabu hiyo.

Kiungo Azzedine Ounahi ambaye amefanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka jana nchini Qatar amekua akivitoa udenda vilabu mbalimbali barani ulaya na mabingwa hao wa Ufaransa wakihusishwa, Lakini klabu hiyo imeweka wazi kwenye mradi wao mchezaji huyo hana nafasi.

Kiungo Azzedine Ounahi ameingia kwenye rada ya vilabu mbalimbali kutokana na uwezo ambao aliionesha kwenye michuano ya kombe la dunia. Huku akifanikiwa kuiwezesha timu yake ya taifa ya Morocco kua timu ya kwanza ya Afrika kufika nusu fainali ya michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live