Paris St-Germain imeambulia kipigo cha pili kwenye Ligi baada ya kukubali kufungwa goli 3-1 kutoka kwa Nantes katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1 mtanange uliopigwa Jumamosi ya Februari 19.
Kwenye mechi hiyo PSG walikosa penati ambayo ingewapa alama moja baada ya Neymar Jr kukosa, ambapo Neymar mwenyewe alifunga goli la kwanza kwa PSG.
Kabla ya kipigo hicho, kocha Mauricio Pochettino na timu yake walikuwa hawajapoteza mchezo wowote tangia mwezi Octoba, lakini bao la Randal Kolo Muani lilitikisa utawala huo.
Quentin Merlin aliongeza bao la pili kwa Nantes wakati ambao bahati ilikuwa kwao kwani walipata tuta ambalo lilikwamishwa na Ludovic Blas.
Unaweza kupongeza ushindi wa Nantes lakini bila kumtaja mlinda mlango Alban Lafont, pongezi zinaweza kuwa na dosari maana alifanya kazi kubwa kuokoa michomo langoni mwake, aliokoa mchomo wa Lionel Messi, Mbappe na Neymar penati.
Nantes wanakwea mpaka nafasi ya 5 wakati PSG wataendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligue 1 kwa tofauti ya alama 13 dhidi ya timu iliyonafasi ya pili Marseille.