Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PRISONS YANG’ARA NYUMBANI

Fef0506354654c1d8e8d177e1dc47ea2.png PRISONS YANG’ARA NYUMBANI

Mon, 15 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAAFANDE wa Tanzania Prisons wameng’ara nyumbani baada ya kuifunga JKT Tanzania bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela Rukwa jana.

Ushindi huo umeipandisha Prisons kwa nafasi moja juu kutoka nafasi ya tisa hadi ya nane na kufikisha pointi 31 baada ya kucheza michezo 23 huku JKT wakiwa katika nafasi ya 15 wakiwa na pointi 24 baada ya kucheza michezo 24.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani na kushambuliana kwa zamu ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko bila kuona lango la mpinzania wake.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 66 Prisons ilipata bao lililofungwa na Samson Mbangula lakini wachezaji wa JKT walilalamika kuwa kabla ya kufunga alikuwa ameotea.

Baada JKT walisazisha lakini mchezaji aliyemalizia kupiga mpira alikuwa ameotea na kumfanya mwamuzi msaidizi namba mbili kulikataa bao hilo.

Baada ya mchezo kumalizika wachezaji JKT wakiwa na benchi la ufundi walionekana kuwalalamikia wamuzi wa mchezo huo ambao walikuwa ni Hery Sasii, Hamis Chang’walu na Hamad Rashid wote wa Dar es Salaam.

Chanzo: www.habarileo.co.tz