Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PRISONS YAAPA KULIPA KISASI KWA YANGA

62e6238128625e7754ce36ac3679770a.jpeg PRISONS YAAPA KULIPA KISASI KWA YANGA

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya Tanzania Prisons imeapa kuvunja rekodi ya Yanga kutokufungwa tangu Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ulipoanza na kulipa kisasi cha kuharibiwa rekodi yao msimu uliopita.

Tanzania Prisons yenye pointi 21 katika nafasi ya 11, itakuwa mwenyeji wa Yanga inaoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi 43, kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, Rukwa kesho.

Msimu uliopita Yanga ndio ilikuwa timu ya kwanza kuifunga Tanzania Prisons katika Ligi Kuu kwenye mzunguko wa 12 hivyo na wao wamepania kulipa kisasi cha kuharibiwa rekodi yao na Yanga.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba alisema: “Sasa ni zamu yetu kulipa kisasi japo mchezo hautakuwa rahisi lakini tutavunja rekodi ya Yanga ya kutokufungwa ili dhamira yetu itimie,” alisema Kazumba.

“Yanga haijapoteza mechi, tumejipanga kuwa timu ya kwanza kuifunga na kuharibu rekodi hiyo kama walivyotufanyia wao msimu uliopita,” aliongeza Kazumba.

Msimu uliopita, Prisons ilicheza michezo 12 bila kupoteza, lakini Yanga ilikuwa timu ya kwanza kuifunga kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Samora, Iringa, Desemba 27 mwaka jana, kwa bao la Patrick Sibomana.

Wakati Yanga inavunja rekodi ya Tanzania Prisons, ilikuwa imeshinda michezo minne na kutoka sare michezo minane na wao wanataka kuvunja rekodi ya Yanga ambayo imecheza michezo 17, ikishinda michezo 13 na kutoka sare michezo minne.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Yanga, Cedric Kaze alisema wamepata mazingira mazuri ya kufanya mazoezi.

Chanzo: habarileo.co.tz