Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PITSO MOSIMANE: Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika

Pitso Yanga .jpeg Pitso akubali mziki wa Yanga

Sun, 7 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mwenye 'Profile' Pitso Mosimane raia wa Afrika ya Kusini amekiri kuwa Yanga ni miongoni mwa vilabu vikubwa barani Afrika.

Pitso ameyasema hayo muda mchache baada ya kutamatika kwa Tamasha kubwa la Klabu ya Yanga linalojulikana kama 'Siku ya Mwananchi' ambalo alialikwa kushiriki kilele cha Tamasha hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Pitso ameandika;

"Nimetembea takriban 70% ya bara la Afrika, kwa mtazamo wangu, Yanga ni miongoni mwa timu kubwa Afrika"

Kauli hiyo ya Pitso inakuja miezi michache tangu alipoeleza kushangazwa kwake na mwamko wa Mashabiki wa vilabu vya Tanzania baada ya kushuhudia gwaride la Ubingwa wa Ligi Kuu lililofanywa na Yanga, ambalo juzi alikiri kuwa lilipeleka ujumbe duniani.

Pitso alikuwepo jukwaani wakati Yanga ikipoteza kwa magoli 2-0 mbele ya Mabingwa wa Uganda Vipers SC katika kilele cha maadhimisho ya 'Siku ya Mwananchi'

Pitso Mosimane amewahi kuvifundisha vilabu vya Mamelodi Sundowns na Al-Ahly huku kote akifanikiwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live