Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

PICHA 4: Azam FC watambulisha basi jipya, sifa zake kiboko

Matajiri Basi 4 Muonekano wa Basi Jipya la Azam FC

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji, Klabu ya Azam FC, wametambulisha basi jipya ambalo ndilo litakalotumiaka katika usafiri wa mechi zaoo mbali mbali msimu wa 2021/2022.

Basi hilo la Azam ni IRIZAR i6S PLUS.

Irizar ni kampuni ya kutengeneza mabodi ya mabasi iliyopo Hispania, na kutokana na ubora wa mabodi yao, makampuni mengi makubwa ya magari duniani yamefanya kazi na kampuni hii katika magari yao.

Iveco, MAN, Mercedes-Benz, Scania, Volvo na hata Lamborghini yamekua yakifanya kazi na Kampuni hii.

Julai 24th 2021, Irizar walizindua basi lao jipya aina ya IRIZAR i6S PLUS, linalotumia injini na chasis ya Mercedes Benz,

Uzinduzi huu ulifanyika huko Midrand Gauteng Afrika Kusini, kwenye uwanja wa mbio za magari ya langalanga, Kyalami Grand Prix Circuit.

Kampuni ya Irizar imedhamiria kutoa kwa Afrika mabasi ya ubora wa juu kama ule ule inaoutoa kwa masoko mengine yote duniani.

Irizar i6S imekuwa ikizinduliwa mfululizo katika nchi zote za Amerika Kusini, Afrika na Australia, baada ya kutawala soko la Ulaya.

Uzinduzi huo rasmi ulishuhudia utambulisho wa mabasi mapya ya kifahari ya urefu wa mita 14 na 15, ambayo yataongeza nakshi kwa basi familia ya Irizar i6.

Familia ya IRIZAR i6 kwa sasa imekamilika kwenye soko la barani Afrika, ikijumuisha mabasi aina ya i6, i6 PLUS, na i6 FRONT ENGINE.

Irizar i6S Plus imezunduliwa Julai 24, 2021, Oktoba 2, 2021 Azam FC wamelishusha kwenye ardhi ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania.

Timu ya taifa ya England, Three Lions, inatumia basi aina ya Irizar i6, ambalo ni toleo la nyuma mara tatu ya hili la Azam FC.







Muonekano wa Basi Jipya la Azam FC

Chanzo: www.tanzaniaweb.live