Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ozil awapa maua yao Maguire, Onana

Ozil Awapa Maua Yao Maguire, Onana Ozil awapa maua yao Maguire, Onana

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa ‘klabu’ ya Arsenal, Mesut Ozil, amewapa maua yao wachezaji wawili kutoka ‘timu’ ya Manchester United, mlinda mlango Andre Onana, na beki Harry Maguire baada ya kuonesha kiwango kizuri kufuatia mchezo wa jana ‘Ligi’ ya mabingwa Ulaya.

Ozil ametoa sifa hizo baada ya siku za hivi karibuni Onana na Maguire kukosolewa kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kutoisaidia ‘timu’ ya Man United kupata matokeo mazuri.

Kupitia ukurasa wake wa X wa Ozil ameandika ujumbe usemao “Harry Maguire na Andre Onana wamestahili hilo, wamewanyamazisha waliokuwa wanawachukia”

Maguire na Onana waliupiga mwingi kufuatia mchezo wao na Copenhagen FC uliochezwa katika uwanja wa Old Trafford na kuondoka na ushindi wa bao 1-0 huku Migaire akitupia bao pekee na Onana kuokoa 'penati' dakika za mwishoni. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live